IQNA

Iran kuajiri waalimu 5000 wapya wa Qur'ani

22:03 - February 06, 2012
Habari ID: 2269851
Waziri wa Elimu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hamid Ridha Haji Babai amesema walimu 5000 wapya wa Qur'ani wataajiriwa kote nchini.
Akizungumza na IQNA, amesema hatua hii ni katika fremu ya mpango wa wizara yake wa kupanua shughuli za Qur'ani na kuinua kiwango cha utaalamu katika mafunzo ya Qur'ani.
Ameongeza kuwa Rais Ahmadinejad ameidhinisha mpango huo wa kuwaajiri walimu 5000 wa Qur'ani na kuongeza kuwa serikali ina azma kamili ya kuunga mkono mpango huo.
Haji Babai amesema hivi sasa kunafanyika mkakati wa kuwatambua walimu bora na wenye uwezo ili kuanza kazi katika mikoa 32 nchini.
Pia ameashiria Mpango wa Kitaifa wa Kuhifadhi Qur'ani na kusema hadi sasa wanafunzi milioni 2.2 wamejiandikisha kwa lengo la kushiriki katika mpango huo na idadi hiyo inatazamiwa kupindukia milioni tatu. Amesema mpango huo utatekelezwa katika shule 120,000 kote nchini.

946507

946507
captcha