IQNA

Maadhimisho ya maulidi ya Mtume (saw) yafanyika katika bunge la Iraq

19:52 - February 07, 2012
Habari ID: 2270633
Maadhimishi ya maulidi ya Mtume Mtukufu (saw) yalifanyika jana Jumatatu katika bunge la Iraq.
Maadhimisho hayo yalifanyika katika ukumbi mkuu wa bunge hilo kwa kuhudhuriwa na Spika Usama an-Nujeifi. Katika maadhimisho hayo maisha na fadhila za Bwana Mtume (saw) zilitajwa na kusisitizwa kwamba mtukufu huyo ni Mtume ambaye alijaza nyoyo na akili za wanadamu kwa nuru na rehema.
Akizungunza katika sherehe hiyo, Spika an-Nujeifi alisisitiza udharura wa kufuatwa nyayo na mafundisho ya Mtukufu huyo. Amesema Bwana Mtume (saw) aliweza kuikomboa jamii ya mwanadamu kutokana na matatizo mengi yaliyokuwa yakiikumba katika zama zake kupitia maadili na sifa zake njema. Ameongeza kwamba Iraq hii leo inahitajia kulindwa haki za binadamu na demokrasia kuliko wakati mwingine wowote na kwamba kutozingatiwa jambo hilo kutailetea nchi hiyo matatizo mengi.
Ibrahim al-Jaafari, mkuu wa chama cha Muungano wa Kitaifa wa Iraq na Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo alisisitiza juu ya umuhimu wa kujiepusha na mitazamo ya kibaguzi na taasubi za kikabila na kimadhehebu nchini humo. 949115
captcha