Kwa mujibu wa tovuti ya Qur'an, mashindano hayo yaliyoandaliwa na vituo vya Kiislamu vya IIC na MAC yamepangwa kufanyika katika Kituo cha Vijana na Jamii ya Kiislamu cha Canada. Washiriki wa mashindano hayo watatakiwa kuhifadhi juzuu ya kwanza hadi ya 10, 21 hadi 30, 1 hadi 5, 28 hadi 30, 29 hadi 30, juzuu ya 30, nusu ya juzuu ya kwanza na kiraa ya Qur'ani nzima.
Mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka yanalenga kuimarisha uhusiano wa jamii ya Kiislamu na mafundisho ya Qur'ani, kunyanyua kiwango cha Waislamu kuhusiana na umuhimu wa kitabu hicho cha mbinguni na kuongeza hamu ya watu wanaotaka kuzingatia zaidi mafundisho ya kitabu hicho pamoja na hifdhi na usomaji wake.
Duru ya 10 ya mashindano hayo ilifanyika mwanzoni mwa mwaka huu kwa ushirikiano wa Kituo cha Kiislamu cha Canada, Taasisi ya Kiislamu ya Amin na Madrasa ya Kiislamu ya Iqra. 949404