IQNA

Hizbullah ya Lebanon yasisitiza juu ya kudumishwa mapambano

16:02 - February 08, 2012
Habari ID: 2271137
Sheikh Nabil Qawouq, Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah amesema kuwa njama za maadui wa Uislamu zinatoa udharura wa kushikamana na stratijia ya mapambano kwa ajili ya kulinda Lebanon na kukombolewa mashamba ya Shab'a na Kufr Shuba.
Akizungumza hapo siku ya Jumatatu katika mji wa Saida kusini mwa Lebanon, Sheikh Qawouq amesema kuwa kuna haja ya kuimarishwa stratijia ya mapambano ya Kiislamu kwa lengo la kulinda kujitawala kwa Lebanon katika kukabiliana na hujuma ya aina yoyote ya ghafla kutoka kwa utawala haramu wa Israel.
Akizungumzia ukakamavu wa harakati ya mapambano ya Hizbullah katika mazingira tofauti nchini Lebanon, Mashariki ya Kati na katika ngazi za kimataifa, Sheikh Qawouq amesisitiza kuwa hakuna siku yoyote ambapo harakati hiyo ya Kiislamu itashirikiana na madola ya kibeberu ya Magharibi katika kudhamini maslahi yao haramu katika nchi za Kiislamu zikiwemo Lebanon, Syria, Palestina na Iraq.
Huku akiashiria uungaji mkono wa Hizbullah kwa marekebisho ya kisiasa yanayofanywa na viongozi wa Syria kwa shabaha ya kuimarisha misingi ya demokrasia nchini, Sheikh Qawouq amesema kwamba njama zinazotekelezwa na madola ya Magharibi dhidi ya serikali ya Damascus zinakusudiwa kuzusha ghasia za muda mrefu si nchini humo tu bali katika nchi zote za Mashariki ya Kati.
Amekosoa vikali msimamo wa hivi karibuni wa nchi za Kiarabu wa kuunga mkono siasa za kichochezi za nchi za Magharibi dhidi ya Syria na kusema kuwa msimamo huo hatari unahudumia tu maslahi na siasa za kujipanua za utawala haramu wa Israel katika eneo hili kwa madhara ya nchi za Kiislamu na Kiarabu. 949962
captcha