Kwa mujibu wa gazeti la Al Sharq, sherehe za kuzindua taasisi hiyo zimehudhuriwa na Gheith ibn Mubarak Al Kawari, Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu Qatar pamoja na wataalamu wa Qur'ani na wanazuoni kadhaa wa Qatar katika nchi za kigeni.
Taasisi hiyo itakayosimamiwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu inalenga kuhuisha na kustawisha utamaduni wa kusoma na kuitafakari Qur'ani Tukufu, kutekeleza mafundisho yake na kuimarisha uhusiano wa watu na kitabu hiki kitukufu. Taasisi hiyo pia inalenga kueneza sira ya Mtume Muhammad SAW.
949053