IQNA

Mamilioni ya Wairani wajitokeza kuadhimisha miaka 33 ya Mapinduzi ya Kiislamu

14:36 - February 12, 2012
Habari ID: 2272384
Mamilioni kwa mamilioni ya wananchi wa Iran wamejitokeza katika maandamano ya kuadhimisha miaka 33 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yaliyopata ushindi mwaka 1979 kwa uongozi wa Imam Ruhullah Khomeini MA.
Mjini Tehran waandamanaji wamesisitiza juu ya udharura wa kusimama kidete kwa ajili ya kuyatetea na kuyahami Mapinduzi ya Kiislamu na matukufu yake. Maandamano hayo ambayo yaliwashirikisha wake kwa waume, wakubwa kwa wadogo, vijana kwa wazee na hata watoto wadogo yameshuhudiwa pia katika kila kona ya Iran.
Sisitizo kubwa la wananchi wa Iran katika maandamano ya tarehe 22 Bahman sawa na tarehehe 11 Februari ni kutosalimu amri mbele ya vitisho, vikwazo na chokochoko za madola ya kibeberu yakiongozwa na Marekani.
Zaidi ya waandishi habari 15,000 wa ndani na zaidi ya waandishi 200 kutoka nje ya Iran wameakisi maandamano ya kuadhimisha miaka 33 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Mjini Tehran waandamanaji walisoma azimio mwishoni mwa maandamano yao azimio ambalo limelaani njama za kishetani na za ubeberu wa kimataifa pamoja na za viongozi vibaraka wa Marekani katika Mashariki ya Kati dhidi ya Iran.
951258
captcha