Rais Ahmadinejad amesema hayo hapa mjini Tehran mbele ya hadhara kubwa ya mamilioni ya Wairani katika maadhimisho ya miaka 33 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusisitiza kwamba, daima mahudhurio ya wananchi katika medani mbalimbali yamekuwa yakikwamisha njama za mabeberu na madola yanayopenda kujitanua.
Amesenma, mahudhurio ya wananchi katika medani mbalimbali ni miongoni mwa matunda makubwa ya Mapinduzi ya Kiislamu.
Rais Ahmadinejad ameongeza kuwa, watu ambao leo wako kando ya Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya wakifanya hima ya kuuokoa utawala wa Kizayuni wa Israel huku wakiyashinikiza mataifa yanayopigania uhuru na ambayo yanaunga mkono muqawama wanapaswa kutambua kwamba, kesho ni zamu yao kukumbwa na hatima mbaya iliyowapata viongozi madikteta.
Rais wa Iran ameashiria maendeleo makubwa yaliyopigwa na taifa hili katika nyuga za kielimu na kubainisha kwamba, kusimama kidete taifa hili kutalifanya lifanikiwe kufikia malengo yake yote liliyojipangia.
951332