IQNA

Wizara ya Wakfu ya Saudi Arabia yatakiwa izingatie taasisi za Qur'ani za Mashia

14:56 - February 12, 2012
Habari ID: 2272534
Mwanafikra wa Kiislamu ambaye pia ni Imamu wa Swala ya Ijumaa ya mji wa Qatif nchini Saudi Arabia ameitaka Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya nchi hiyo kuzingatia taasisi za kidini na Qur'ani za Mashia wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa kanali ya habari ya Raswid, hayo yamesemwa na Hujjatul Islam wal Muslimeen Hassan Saffar katika kikao kilichofanyika ofisini kwake kwa ajili ya kutoa ripoti ya kila mwaka kuhusiana na hali ya haki za kidini nchini Saudia.
Kikao hicho kimeitaka Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Saudia kuzingatia na kusaidia kutatua matatizo mengi yanayozikumba taasisi za kidini, kiutamaduni pamoja na vituo na kamati za kimadhehebu za Mashia.
Sheikh Saffar amesema kuwa hadi sasa hakuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa na wizara hiyo kwa lengo la kusaidia kukarabati au kujenga misikiti ya Mashia katika maeneo yaliyo na wakazi wengi wa Kishia. Amesema licha ya kuwepo kamati nyingi za mafunzo ya Qur'ani Tukufu katika maeneo ya Mashia lakini hakuna msaada wowote unaotolewa na wizara iliyotajwa kwa kamati hizo.
Shekh Saffar ameendelea kusema kuwa utawala wa Saudia unapasa kutenga bajeti maalumu ya kusaidia taasisi na vituo vya Qur'ani katika maeneo ya Mashia wa nchi hiyo kama unavyofanya kuhusiana na vituo vingine vya Qur'ani ndani na nje ya nchi hiyo. 951105
captcha