Kikao hicho kiliandaliwa na Chuo cha Kiislamu cha Imam Sadiq AS mjini Dar-es-Salaam na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya Waislamu nchini Tanzania.
Kikao hicho kilianza kwa kisomo cha Qur'ani Tukufu na kufuatiwa na qasida zilizotayarishwa na wanafunzi wa chuo hicho cha kidini.
Hafla hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 17 Rabi'ul Awwal na kuhutubiwa na mkuu wa chuo hicho Sheikh Hemed Jalala ambaye alizungumzia shakhsia ya Mtume SAW na Imam Ja'afar Sadiq AS.
Hafla hiyo ya Maulidi ni kati ya sherehe ambazo hufanywa na Waislamu wa Tanzania. Sherehe za Maulidi nchini Tanzania sawa na maeneo mengine ya Afrika Mashariki huanza 12 Rabi'ul Awwal na kuendelea kwa miezi miwili katika miji mbalimbali ya eneo hilo.
951820