Askari jeshi wa nchi hiyo wakisaidiwa na wa kigeni wamekandamiza na kujaribu kuwatawanya waandamanaji waliofika katika medani hiyo.
Wananchi wa Baharin licha ya kukandamizwa na jeshi la Bahrain ambalo linasaidiwa na askari vamizi wa Saudi Arabia, lakini wamekuwa wakakamavu mbele ya ukandamiza huo wa kinyama na kuendelea kupigania haki zao za kimsingi zikiwemo za uhuru wa kushiriki kwenye uchaguzi wa kuainisha mustakbali wao, demokraisa, kufikishwa mahakamani wahusika wa vitendo vya jinai na hatimaye kuondolewa madarakani watawala wasiofaa.
Licha ya utawala wa Aal Khalifa kufanya unyama na jinai dhidi ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo lakini wananachi wamekuwa wakiimarisha harakati za kutetea haki zao kutoka kwa utawala huo bila woga wowote.
Akizungumzia jambo hilo, Ibrahim al-Iradi mwanaharakati wa kisiasa wa Bahrain amesema kwamba watawala wa nchi hiyo ndio wanaopasa kubeba lawama za hali na mgogoro unaoshuhudiwa sasa nchini humo. Amesema lengo la wananchi kurejea katika Medani ya Lulu ni kufuatilia matakwa yao kutoka kwa watawala wa nchi hiyo.
Al Iradi ameongeza kuwa maandamano, malalamiko na uhuru wa kujieleza ni haki za wazi za wananchi wa Bahrain zisizopasa kujadiliwa kwa sababu zinakwenda sambamba na maazimio ya kimataifa ambayo utawala wa Bahrain unajivunia kuyatia saini lakini hauyatekelezi. 953014