IQNA

Kituo cha pili cha redio ya Kiislamu ya al-Bayan chafunguliwa Ivory Coast

16:12 - February 15, 2012
Habari ID: 2274600
Kituo cha pili cha redio ya Kiislamu ya al-Bayan kilifunguliwa jana Jumanne katika mji wa Gagnoa, Magharibi mwa Ivory Coast.
Kwa mujibu wa tovuti ya AIP sherehe za ufunguzi wa kituo hicho zilifanyika jana alasiri katika msikiti wa Ijumaa wa Gagnoa ambapo Imam Sise Jigiba, mkurugenzi wa kituo hicho pamoja na Waislamu wa mji huo walishiriki.
Akizungumza mbele ya hadhara ya watu walioshiriki katika sherehe hizo, Imam Jigiba alisema kuwa ana matumaini kwamba kituo hicho cha redio kitasaidia pakubwa katika kuimarisha maelewano, upendo, kuvumiliana na udugu miongoni mwa wakazi wa mji wa Gagnoa na vilevile kuimarisha utamaduni wa kufanyika mazungumzo baina ya wafuasi wa dini tofauti katika mji huo na nchi nzima ya Ivory Coast.
Amesema redio hiyo haitazingatia ukabila, rangi wala jinsia ya watu bali itazingatia tu masuala ya kuimarisha utamaduni wa udugu unaosisitizwa katika Uislamu katika jamii ya nchi hiyo.
Ni vyema kuashiria hapa kwamba kituo cha kwanza cha redio hiyo kipo mjini Abidjan ambao ni mji mkuu wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Wasimamizi wa redio hiyo wamechukua uamuzi wa kuanzisha kituo cha pili magharibi mwa nchi hiyo kutokana na mahitaji ya Waislamu wa eneo hilo. 953755
captcha