IQNA

Kushadidi ukatili wa utawala wa kifalme Bahraini

12:12 - February 16, 2012
Habari ID: 2275030
Vyanzo vya habari vinaripoti kushadidi mapigano makali baina ya wanamapinduzi wa Bahrain na vikosi vya Aal Khalifa.
Vikosi vya Aali Saud vikishirikiana na vikosi vya Aal Khalifa vimewavyatulia risasi na gesi ya sumu waandamanaji waliokuwa wakielekea Medani ya Shuhadaa.
Idadi kamili ya waandamanaji waliouawa katika Medani ya Shuhadaa na vikosi hivyo vya Aal Khalifa na Aal Saud haijajulikana hadi sasa.
Utawala wa Aal Khalifa, siku ya Februari 14 inayosadifiana na mwaka mmoja tangu zilipoanza harakati za mapinduzi ya tarehe 14 Februari mwaka jana, ulishadidisha ukandamizaji na kuwakanyaga kwa magari waandamanaji wanaopinga utawala huo na kusababisha mauaji katika kitongoji cha Bani Jamra.
Vikosi vya utawala wa Aali Khalifa pia vimewafyatulia gesi yenye sumu wanafunzi katika kisiwa cha Sitra na kuwazuia wakazi wa eneo hilo kushiriki katika maandamano yaliyokuwa yakielekea Medani Shuhadaa au Medani ya Lulu ya zamani.
Hatua ya kuwazuia watu kuitikia wito uliokuwa unawata kufika katika Medani ya Shuhada imepelekea vikosi vya Aal Khalifa na askari vamizi wa Saudia kuyashambulia maandamano ya amani katika maeneo ya al Akri, Bani Jamrah, al Deyhi, al Salhiya, Udhari, al Sanabis na Biladul Qadim.
Vyombo vya habari katika maeneo hayo vimeripoti kuwa, mapema leo asubuhi kulikuwa na maandamano makubwa kuelekea Medani Shuhadaa ambayo yaliwashirikisha raia wengi wa Bahrain waliojitolea nafsi zao na wengine wakiwa wamevaa sanda.
Viongozi kadhaa wa kisiasa akiwemo Muhammad al Hayki na Muhammad Ja'far walitiwa mbaroni na vikosi hivyo vya Aali Khalifa walipokuwa wakijaribu kufika katika Medani ya Shuhadaa.
Kufuatia hali hiyo Ayatullah Shekh Muhammad Sanad ambaye ni mmoja wa viongozi wa vijana wanamapinduzi wa Bahrain amewataka wananchi kuendelea na mapambano na kusimama imara katika maeneo yao.
Wakati huo huo viongozi wa chama cha Kiislamu cha al Wafa pia wamewataka wanamapinduzi kujitokeza kwa wingi barabarani na viwanja mbalimbali vya Manama na kuendeleza upinzani wao dhidi ya utawala wa Aal Khalifa.
Kushadidi doria inayofanywa na vyombo vya usalama vya utawala wa Aal Khalifa na vikosi vamizi vya Aal Saud hakukuwazuia wananchi kufika kwa wingi katika Medani ya Shuhadaa.
Wakati huo huo mwakilishi wa jumuiya ya Kiislamu ya al Wifaq ambacho ni chama kikubwa zaidi cha upinzani nchini Bahrain, Matar Ibrahim Matar amesema kuwa, kwa muda wa mwaka mmoja sasa wananchi wa Bahrain wamesimama kidete dhidi ya ukandamizaji mkubwa wa vikosi vya utawala wa nchi hiyo, na kuongeza kuwa, wananchi hao hawatakaa kimya mpaka waung'oe madarakani utawala wa kiimla wa nchi hiyo.
Amesisitiza kuwa pamoja na kupita muda mwingi wananchi wa Bahrain hawataacha kupigania matakwa yao ya msingi.
Itakumbukwa kuwa tangu kuanza mwamko wa Kiislamu wa tarehe 14 Februari 2011 nchini humo vikosi vya utawala kibaraka wa Aal Khalifa vimewaua mamia ya raia na kuwajeruhi maelfu wengine huku idadi kamili ya waliokamatwa na kupelekwa pasipojulikana ikiwa haieleweki.
953727
captcha