Sherehe za kuwaenzi washindi hao zitafanyika leo jioni katika ukumbi mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Wizara ya Utamaduni, Vijana na Maendeleo ya Jamii mjini Ras al-Kheima. Mgeni wa heshima katika sherehe hizo atakuwa Sheikh Saud bin Saqar al-Qassimi, mtawala wa Ras al-Kheima.
Akizungumzia mashindano hayo, Sheikh Amr bin Abdul Aziz al-Qasimi, Katibu Mkuu wa duru ya 12 ya Mashindano ya Kitaifa ya Imarati amesema kuwa wanafunzi 80 kutoka shule za serikali na binafsi pamoja na vituo vya Qur'ani wameshiriki katika mashindano hayo.
Ameongeza kuwa kamati tano za waamuzi wa Qur'ani zilichaguliwa kuyasimamia.
Mashindano hayo yalifanyika katika vitengo vya hifdhi ya Qur'ani nzima, hifdhi ya juzuu 20 ikiandamana na tajwidi, juzuu 10 na tajwidi, juzuu 5 na tajwidi na hifdhi ya juzuu 3 na tajwidi. 953898