Kituo cha Kiislamu cha Uingereza kimeandaa masomo maalumu ya Qur'ani Tukufu na sheria za Kiislamu kwa Waislamu wapya waliosilimu katika siku za hivi karibuni katika Kituo cha Kiislamu kilichoko katika mji mkuu wa Uingereza, London.
Kwa mujibu wa tovuti ya IC-EL masomo hayo ambayo yamekuwa yakiendeshwa kwenye kituo hicho tokea mwezi Novemba mwaka uliopita yataendelea hadi tarehe 25 mwezi ujao wa Machi.
Wanafunzi wanaoshiriki masomo hayo ya kujifunza Qur'ani Tukufu wanashiriki katika makundi matatu ya utangulizi, ya kati na ya juu. Katika kundi la utangulizi, wanafunzi watajifunza lugha ya Qur'ani na wale wa kundi la kati na la juu watajifunza sheria za usomaji Qur'ani na tajwidi.
Masomo hayo yatakuwa yakitolewa kila siku ya Jumamosi katika kituo kilichotajwa cha Kiislamu. Mijadala ya wazi kuhusiana na Qur'ani pia itafanyika pambizoni mwa masomo hayo. 955156