Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah Sayyid Hassan Nasrallah amesema Marekani, Utawala haramu wa Israel, baadhi ya nchi za Kiarabu na Al Qaeda ndio wachochezi wakuu wa ghasia nchini Syria kwa lengo la kumpindua Rais Bashar al Assad.
Sayyid Nasrallah ameyasema hayo Alkhamisi katika hotuba iliyorushwa hewani kupitia televisheni mjini Beirut kwa mnasaba wa kukumbuka mwaka wa nne tokea auawe shahidi kamanda mwandamizi wa Hizbullah Imad Mughniyah.
Katka hafla hiyo wamenziwa pia mashahidi Sayyid Abbas Al-Moussawi na Sheikh Ragheb Harb. Kiongozi wa Hizbullah ameongeza kuwa Israel inafadhilisha kundi lolote kuwa madarakani Syria kuliko serikali ya Bashar al Asad. Sayyid Nasrallah amezikosoa baadhi ya nchi za Kiarabu zenye uhasama dhidi ya Syria. Amesema nchi hizo za Kiarabu zinasema hakuna wakati wa kutafuta suluhisho la kisiasa Syria wakati ambao zinakubali kufanya mazungumzo na utawala haramu wa Israel.
Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema Syria inasakamwa kwa sababu Rais Bashar al Assad kamwe hajawahi kusalimu amri mbele ya matakwa ya Marekani na utawala haramu wa Israel.
Sayyid Nasrallah amesema uhusiano wa Hizbullah na Syria ni wa kistratijia. Ameelezea matumaini yake kuwa Syria itaanzisha marekebisho makubwa ili kuzima njama za Wamagharibi dhidi ya nchi hiyo.
954822