Taarifa iliyotolewa na Hizbullah na Amal imesema kuwa Syria inalengwa kwa mashambulizi ya nchi za kibeberu kutokana na himaya na uungaji mkono wake kwa wananchi wa Palestina wanaopigania haki zao.
Taarifa hiyo imesema kuwa mbali na kuwaunga mkono na kuwasaidia wananchi wa Palestina, Syria pia inahami na kuunga mkono mapambano ya wananchi wa Lebanon dhidi ya utawala ghasibu wa Israel, suala ambalo linawakasirisha maadui walioamua kuelekeza mishale yao dhidi ya nchi hiyo.
Hizbullah na Amal zimetangaza uungaji mkono wao kwa marekebisho yanayotekelezwa na Rais Bashar Assad wa Syria na kusema kuwa mbinu hiyo ndiyo njia pekee ya kukabiliana na fitina za ndani na njama za kigeni. 956382