Maelfu ya Waafghani wameandamana kuelekea katika kituo cha jeshi la anga cha Bagram huko kaskazini mwa Kabul na kukizingira kituo hicho.
Kufuatia maandamano hayo kamanda wa jeshi la Marekani nchini Afghanistan Jenerali John Allen amesema kuwa ameamuru kukamatwa na kusailiwa askari wa Marekani waliohusika na uchomaji wa vitabu vya Kiislamu ikiwemo Qur'ani Tukufu.
Allen pia amemuomba sahamani Rais wa Afghanistan, serikali na wananchi wa nchi hiyo kutokana na kitendo hicho.
Polisi ya Kabul imetangaza kuwa Waafghani zaidi ya elfu mbili wangali wanazingira kituo cha kijeshi cha Marekani cha Bagram.
Sambamba na maandamano hayo kumefanyika maandamano mengine katika miji mbalimbali ya Afghanistan ikiwa na pamoja na katika barabara ya Jalalabad, makao makuu ya vituo vya kijeshi vya NATO kulalamikia kitendo cha askari wa Marekani cha kuchoma moto kitabu kitakatifu cha Qur'ani. 957705