IQNA

Hizbullah yalaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu

16:51 - February 22, 2012
Habari ID: 2279117
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imelaani kitendo cha askari wa Marekani nchini Afghanistan cha kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu katika kituo cha jeshi la anga cha Bagram huko kaskazini mwa mji wa Kabul.
Taarifa iliyotolewa na Hizbullah imesema kuwa kitendo cha askari wa Marekani cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu ni jinai mpya inayodhihirisha dharau kubwa ya Wamarekani na Wazayuni kwa matukufu ya Kiislamu.
Taarifa hiyo imesema kuwa dharau hiyo ya Wamarekani na Wazayuni inaonesha jinsi wahalifu hao wanavyodharau na kupuuza matukufu ya Waislamu zaidi ya bilioni moja kote duniani.
Hizbullah imesema kuwa dharai hiyo ya askari wa Marekani dhidi ya kitabu kitakatifu cha Qur'ani inafanyika sambamba na vitendo vya kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu vya walowezi wa Kizayuni dhidi ya matukufu ya Kiislamu huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Taarifa ya Hizbullah imesema kufanyika kwa wakati mmoja dharau hizo za Wamarekani na Wazayuni kunafichua mpango wa kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati na kufanya njama dhidi ya Waislamu.
Imesema hatua hiyo ya askari wa Marekani nchini Afghanistan ni kinyume cha mafundisho ya dini zote za mbinguni.
Hizbullah imewataka Waislamu kote duniani kupaza sauti zao dhidi ya hatua kama hizo na kulaani vitendo vyote vinavyovunjia heshima matukufu ya Kiislamu na Kikristo.
Maelfu ya wananchi wa Afghanistan leo wamefanya maandamano kwa siku ya pili mfululizo wakipinga kitendo cha askari wa Marekani nchini humo ambao wamevunjia heshima na kuchoma moto nakala kadhaa za kitabu kitakatifu cha Qur'ani. 958164

captcha