Tovuti ya Bloomberg imeripoti kuwa maandamano na mikusanyiko ya maelfu ya wananchi wenye hasira wa Afghanistan dhidi ya kitendo cha askari wa Marekani cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu yamewalazimisha maafisa wa Marekani kufunga ubalozi wao mjini Kabul.
Ubalozi wa Marekani Afghanistan umetangaza kuwa ofisi zake zimefungwa hadi hapo baadaye na umewataka wafanyakazi wake wote kufika ubalozini hapo haraka iwezekanavyo.
Maafisa wa Marekani nchini Afghanistan pia wamewapiga marufuku wafanyakazi wa Kimarekani kufanya safari katika mji wa Qandahar ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Afghanistan.
Askari wa Marekani katika kambi ya jeshi la anga ya Bagram jana walichoma moto vitabu vya Kiislamu zikiwemo nakama za kitabu kitakatifu cha Qur'ani. 958640