IQNA

Mashindano ya 51 ya Qur'ani kufanyika Qatar

17:44 - February 22, 2012
Habari ID: 2279146
Duru ya 51 ya mashindano ya hifdhi ya Qur'ani tukufu ya wanafunzi yamepangwa kufanyika tarehe 11 Machi katika mji mkuu wa Qatar, Doha.
Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar imetangaza kuwa lengo la mashindano hayo ni kuwahamasisha wanafunzi wa shule mbalimbali kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu.
Mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka yanafanyika kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi hadi sekondari na kila kitengo kimeainishiwa sura maalumu za kuhifadhi. 958526

captcha