IQNA

'Tuhuma kuwa Iran inalengo la kueneza Ushia Misri hazina msingi'

21:09 - February 22, 2012
Habari ID: 2279180
Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuyakurubisha Madhehebu ya Kiislamu Ayatullah Muhammad Ali Tas'khiri amesema kuwa, tuhuma zinazoenezwa kwamba Iran inafanya juhudi za kueneza Ushia nchini Misri hazina msingi wowote.
Akizungumza mjini Tehran, amesema mahusiano na mshikamano wa kiutamaduni baina ya Iran na Misri kamwe hautakatika. Ameongeza kuwa pamoja na kuwemo mshikamano huo zipo njama za mabaki ya utawala wa Mubarak za kutaka kuudhoofisha, sambamba na njama za maadui dhidi ya Umma wa Kiislamu.
Amesema uhusiano wa Iran na Misri unazidi kuimarika katika nyanja tofauti.
Ameyataka madhehebu ya Kiislamu kwa pamoja kudumisha mshikamano na udugu, na kusaidiana ili kukurubisha michango ya kimawazo, huku umoja ukiwa ndio msingi katika masuala mbalimbali na kutatua changamoto zinazoukumba Umma huu.
958654
captcha