Kwa mujibu wa tovuti ya CPI, askari hao waliingia na kupekua sehemu tofauti za msikiti huo. Walowezi wa Kizayuni nao pia waliingia msikitini humo na kufanya kama walivyofanya askari hao wa Kizayuni huku askari wengine wakiwa wanawalinda na kudhibiti hali ya mambo nje ya msikiti huo.
Askari zaidi wa utawala huo walitekeleza hatua kali za usalama katika milango yote ya kuingilia msikiti hapo huku wakichunguza kwa makini vitambulisho vya vijana wa Kipalestina waliokuwa wakiingia msikitini humo.
Baada ya kuona kitendo hicho cha kichokozi, Waislamu wa Palestina waliingia katika msikiti huo ili kutetea kibla hicho cha kwanza cha Waislamu.
Katika siku za hivi karibuni vyama na makundi ya kibaguzi ya Wazayuni na Mayahudi yamekuwa yakiwachochea wafuasi wao waingie kwenye msikiti huo na kuuvunjia heshima. 958551