IQNA

Onyo la maulama wa Kishia wa Saudia dhidi ya watawala wa nchi hiyo

17:46 - February 25, 2012
Habari ID: 2280430
Zaidi ya wanazuoni mashuhuri 40 wa Saudi Arabia wametoa taarifa wakilaani kuendelea kwa ukandamizaji wa watawala wa nchi hiyo dhidi ya raia wanaofanya maandamano ya amani ya kupigania haki zao.
Wanazuoni hao 41 wa mkoa wa Ahsaa wamesema ukandamizaji huo hauwezi kuvumiliwa na wamewataka watawala wa Riyadh kuanzisha mara moja uchunguzi wa kina kuhusiana na mauaji ya vijana wa Kishia nchini humo.
Sehemu moja ya taarifa hiyo imewataka watawala wa Saudia kuondoa vituo vya upekuzi vilivyowekwa katika maeneo ya kuingia katika miji ya Mashia na pia kuondoa marufuku ya ujenzi wa misikiti na huseinia za Mashia pamoja na kuheshimu matukufu yao. Wamesema kuendelea kwa ukandamizaji na uonevu huo wa watawala wa Saudia dhidi ya Mashia kutazidisha tu mgogoro wa nchi hiyo.
Mambo mengine yanayofuatiliwa na wanazuoni hao wa Kishia ni kuondolewa marufuku ya kuchapishwa vitabu vya Mashia na pia kufuta matusi na uvunjiwaji heshima itikadi za Kishia katika vitabu vya masomo nchini humo. Wamesisitiza kwamba kupuuzwa kwa matakwa hayo na kuendelea kukandamizwa Mashia kutazidisha mgogoro wa nchi hiyo. 959268
captcha