Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni wa Kiislamu ISESCO, jana Ijumaa lilitoa taarifa ya kulaani mashambulio ya umwagaji damu yaliyofanywa na magaidi nchini humo siku ya Alkhamisi iliyopita.
Taarifa hiyo imeyataja mashambulio hayo yaliyotekelezwa katika mikoa kadhaa ya Iraq na kupelekea watu zaidi ya 400 kupoteza maisha yao na kujeruhiwa kuwa ni jinai isiyosamehewa.
Taarifa hiyo imesema kuwa ugaidi huo unatekelezwa na magaidi kwa shabaha ya kuvuruga utulivu wa Iraq na umoja wa watu wa nchi hiyo.
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo ya ISESCO imesema kwamba walengwa wa vitendo hivyo vya ugaidi si serikali na taifa la Iraq tu bali ni Waislamu wote kwa sababu lengo la ugaidi ni kudhamini maslahi ya maadui katika ulimwengu wa Kiislamu.
Taarifa hiyo imezitaka taasisi na viongozi wa nchi za Kiislamu na hasa wanafikra na wanazuoni kulaani vikali vitendo hivyo vya ugaidi na kuisaidia serikali ya Iraq kupambana na vitendo hivyo kwa lengo la kurejesha nchini humo amani na utulivu wa kudumu. 959563