IQNA

Mahafidhi wa Qur'ani Palestina waenziwa

17:50 - February 25, 2012
Habari ID: 2280446
Mateka wa Kipalestina walioachiwa huru hivi karibuni kutoka kwenye jela za Israel ambao wamehifadhi Qur'ani Tukufu wameenziwa katika mji wa Rafah huko Gaza kwa hima ya Taasisi ya Darul Qur'ani.
Katika sherehe hiyo Taasisi ya Darul Qur'ani na Suna za Mtume (saw) ya Ukanda wa Gaza imewaenzi na kuwatunuku zawadi mahafidhi wa Qur'ani walioachiwa huru kutoka kwenye korokoro za Israel.
Sherehe hiyo iliyofanyika kwenye Msikiti wa al Abrar ilihudhuriwa na Mkuu wa Darul Qur'an Abdurrahman al Jamal, wawakilishi wa bunge la Ghaza, Waziri wa Masuala ya Mateka wa Palestina na raia wengi wa eneo hilo.
Mkuu wa Darul Qur'ani ya Ghaza amesema katika sherehe hiyo kwamba mateka wa Kipalestina waliohifadhi Qur'ani Tukufu katika mashaka na mazingira magumu ya jela za Israel ni mashujaa walioweza kuushinda utawala ghasibu na kuvunja matumaini yake.
Amesema mateka hao walioachiwa huru wanapaswa kutambuliwa kama kigezo kinachohimiza kusoma, kuhifadhi na kujifunza Qur'ani Tukufu.
Mahafidhi 45 wa Qur'ani Tukufu waliokuwa katika korokoro za kutisha za Israel walienziwa na kupewa zawadi katika sherehe hiyo. 959678

captcha