Gazeti hilo litaanza kuchapishwa tena kwa madhumuni ya kushughulikia na kuakisi matatizo na changamoto tofauti zinazoikabili jamii ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Misri.
Akitanagaza habari hiyo, Muhammad ad-Duraini, muasisi wa chama cha al-Ghadir ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Aali Beit (as) la Misri amesema kuwa gazeti hilo licha ya kuakisi masuala ya Kishia pia litakuwa likiakisi masuala tofauti ya kisiasa, kijamii, kiutamaduni na kiuchumi yanayoyahusu makundi yote ya nchi hiyo. Amesema litakuwa likiakisi masuala ya Kishia, Kiarabu na Kiislamu katika kukabiliana na njama za utawala haramu wa Israel.
Ad-Durein amesisitiza kwamba gazeti hilo pia litakuwa likiakisi misimamao ya chama cha al-Ghadir katika kukabiliana na njama zinazofanywa na nchi za Magharibi kwa lengo la kuzusha fitina na mifarakano ya kimadhehebu katika jamii za Kiislamu. 960003