Huku akisisitiza umuhimu wa kudumishwa mapambano ya Wananchi wa Palestina kwa lengo la kukombolewa ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel, Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina amesema kwa mara nyingine tena kwamba taifa hilo linakaribia kukomboa Quds Tukufu na Msikiti wa al-Aqsa.
Kwa mujibu wa tovuti ya kbwindow, Ismail Haniya ambaye alikuwa akizungumza siku ya Ijumaa mbele ya mamilioni ya Wamiri huko katika Msikiti wa az-Zahra mjini Cairo ameyataka majeshi ya nchi za Kiislamu na mataifa huru ya Kiarabu kujitayarisha kuingia katika hatua mpya ya kukombolewa Msikiti wa al-Aqsa. Amesema umma wa Kiislamu unakaribia kuingia katika hatua mpya ambapo kukombolewa Msikiti wa al-Aqsa ni miongoni mwa matukio muhimu ya hatua hiyo.
Amesema katika miaka iliyopita Wamisri wengi waliuawa shahidi katika njia ya kupigania uhuru wa Palestina na kuelezea matumaini yake kwamba nchi hiyo ya Kiislamu itaendelea kuteteta ukombozi wa Palestina na Msikiti wa al-Aqsa kutoka kwenye makucha ya Wazayuni.
Ismail Haniya amesema licha ya kukabiliwa na matatizo mengi lakini Palestina imekataa kuutambua rasmi utawala huo ghasibu na kwamba itaendelea kujitolea katika kutetea msimamo huo. 959808