IQNA

Sheikh Zaghmut akosoa kimya cha watawala wa Kiarabu mbele ya kuvunjiwa heshima Qur'ani

15:50 - February 26, 2012
Habari ID: 2281151
Mwanazuoni mashuhuri wa Lebanon Sheikh Muhammad Namr Zaghmut ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Kiislamu la Palestina nchini Lebanon amekosoa kimya cha watawala wa nchi za Kiarabu mbele ya vitendo vya askari wa Marekani vya kuchoma moto Qur'ani Tukufu na akasisitiza kuwa Waislamu watailinda Qur'ani Tukufu kwa nafsi na roho zao.
Sheikh Muhamamd Namr ameashiria kitendo kiovu cha askari wa Marekani cha kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu katika kituo cha anga cha Bagram nchini Afghanistan na akasema kuwa kitendo hicho kimezusha wimbi la upinzani na malalamiko ya Waislamu wa Afghanistan na maeneo mengine duniani na hadi sasa makumi ya Waislamu wa Afghanistan wameuawa shahidi katika njia ya kutetea kitabu cha Mwenyezi Mungu.
Mwanazuoni huyo wa Kiislamu wa Lebanon amesema mabeberu wa kimataifa hususan Marekani wana kinyongo na uhasama mkubwa dhidi ya Waislamu na wanafanya jitihada za kuwaweka Waislamu mbali na Qur'ani Tukufu.
Sheikh Muhammad Namr Zaghmut amesema kuwa Rais Barack Obama wa Marekani na viongozi wengine wa nchi hiyo ni warongo na wanafiki na wamekuwa wakitoa amri za siri za kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu. Amesisitiza kuwa viongozi wa Marekani wanatoa maneno ya uongo kwa nia ya kuwahadaa Waislamu lakini wanapaswa kuelewa kwamba hakuna Muislamu yeyote mwenye kujiheshimu na mpiganaji wa jihadi anayesadiki madai yao.
Amelaani kimya cha baadhi ya viongozi wa nchi za Kiarabu mbele ya kitendo kiovu cha askari wa Marekani cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu na akasema watawala wa Marekani na Ulaya na washirika wao katika nchi za Kiarabu wameungana katika fikra za Kizayuni na kuongeza kuwa watawala wa baadhi ya nchi za Kiislamu wanaongoza nchi zao kwa jina la Marekani, Uingereza, Ufaransa na utawala ghasibu wa Israel. 960420


captcha