Mashindano hayo yatafanyika katika makundi matatu ya kuhifadhi robo ya Qur'ani Tukufu, nusu ya Qur'ani na Qur'ani nzima kwa makari wasichana na wavulana wenye umri wa miaka zaidi ya 10.
Washiriki watatathminiwa kwa mujibu wa uwezo wao wa kuhifadhi aya za Qur'ani Tukufu na kuchunga kanuni za tajwidi.
Baada ya mashindano hayo washindi wataenziwa kwa kutunikiwa zawadi.
Mashindano hayo yatasimamiwa na kituo cha kusimamia mashindano kati ya vyuo vikuu vya Kiislamu nchini Marekani cha MIST. 959945