IQNA

Mahafidhi wa Qur'ani nzima waenziwa

14:50 - February 27, 2012
Habari ID: 2281557
Sherehe za kuwaenzi mahafidhi 44 wa Qur'ani nzima zilifanyika siku ya Jumamosi tarehe 25 Februari katika mji wa Tripoli nchini Lebanon.
Sherehe hizo zilizoandaliwa na Kamati ya Qur'ani Tukufu ya Lebanon kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur'ani zilisimamiwa na Mufti wa Tripoli, ambapo mahafidhi wa kike na kiume 44 walio na vibali vya hifdhi ya Qur'ani walipongezwa na kushukuriwa. Ahmad Khalid, Mkuu wa Halmashauri ya Masuala ya Kiidara ya Hospitali ya Daru Shifaa ya Lebanon na wanachuo kadhaa wa kike na kiume ambao ni wanaharakati wa masuala ya Qur'ani ni miongoni mwa watu walioshiriki kwenye sherehe hizo.
Baada ya kusomwa ya kadhaa za Qur'ani Sheikh Muhammad Imami, Katibu wa Idara ya Fatuwa ambaye pia ni mwakilishi wa Mufti wa Tripoli aliwasifu mahafidhi wa Qur'ani na kuzungumzia baraka za Qur'ani Tukufu na umuhimu wa kuhudumia kitabu hicho kitakatifu cha mbinguni.
Mahafidhi na wasomaji kadhaa wa Qur'ani walisoma aya kadhaa za kitabu hicho kwa visomo tofauti na hatimaye mahafidhi walioshiriki kwenye sherehe hizo walipewa zawadi nono. Sherehe nyingine ya kuwashukuru na kuwazawadia wanafunzi 34 waliohitimu masomo ya Qur'ani ilifanyika katika mji huo wiki iliyopita. 960868
captcha