IQNA

Kuchoma Moto Qur'ani ni vita dhidi ya Allah

14:30 - February 27, 2012
Habari ID: 2281639
Kitendo cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu kilichofanywa na vikosi vamizi vya askari wa Marekani nchini Afghanistan si tu kuwa ni vita dhidi ya Uislamu na Waislamu, bali ni vita dhidi ya Allah SWT.
Akizungumza na IQNA, ustadhi bingwa wa Qur'ani wa Misri Farajullah Shazli ambaye pi yuko katika Bodi ya Chuo Kikuu cha Al Azhar amesema kuwa: 'Waliotekeleza kitendo hicho wataadhibiwa na Mwenyezi Mungu kwani ana nguvu zisizo na kikomo kote duniani na hakuna anayeweza kusimama dhidi yake'.
Amesema Waislamu hawatachukua hatua yoyote ya kuchoma vitabu vya dini nyinginezo ili kulipiza kisasi.
Ustadh Shazli ameashiria aya ya tisa ya Sura ya Hijr isemayo kuwa: ''Hakika Sisi ndio tulioteremsha Ukumbusho huu (Qur'ani), na hakika Sisi ndio tutao ulinda".
Amesema Qur'ani Tukufu ni neno la Allah SWT na ina kinga kamili na yeyote atakayeivunjia heshima ataangamia.
'Mtu yeyote mwenye imani imara hawezi kunyamazia kimya kitendo cha kuichoma moto Qur'ani,' ameongeza na kutoa wito kwa viongozi wa nchi zote za Kiislamu duniani kulaani vikali kitendo hicho na kuchukua hatua za kivitendo kuzua kurudiwa ushenzi huo katika siku za usoni.
Ustadh Farajullah Shazli pia ameashiria hatua ya Rais Barack Obama wa Marekani ya kuwaomba radhi Waislamu baadaya wanajeshi wake kuchoma moto Qura'ani Tukufu huko Afghanistan na kusema: "Iwapo hatalipa suala hilo uzito na kuwaadhibu wahusika, anapaswa kujua kuwa urais wake hatimaye utafika ukingoni na iwapo hatawajibishwa hapa duniani basi kwa yakini ataulizwa kuhusu aliyoyatenda Siku ya Kiyama'.
960731
captcha