IQNA

Al Azhar yataka askari wa Marekani waondoke Afghanistan

12:07 - February 28, 2012
Habari ID: 2282393
Sheikh Ahmad Tayyib wa al-Azhar nchini Misri amelaani vikali kitendo cha kibaguzi cha askari wa Marekani cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu huko Afghanistan na kutaka askari hao waondoke katika ardhi ya nchi hiyo mara moja.
Sheikh Tayyib amesema kwamba kitendo cha askari hao cha kuchoma moto kitabu kitakatifu cha Waislamu katika kambi yao ya kijeshi huko Bagram ni kitendo cha kinyama na amewataka watawala wa Marekani wawaondoe askari hao katika radhi ya Afghanistan mara moja.
Amesema al-Azhar, bali Waislamu wote duniani, hawawezi kuvumilia kuona Qur'ani ikivunjiwa heshima na kukaa kimya mbele ya kitendo hicho cha dharau bila kuchukua hatua yoyote.
Katika sehemu nyingine ya taarifa yake, Ahmad Tayyib amesema kuwa kuondoka kwa askari wote wa Marekani katika ardhi ya Afghanistan ndiyo njia pekee ya kurejeshwa amani na utulivu katika nchi hiyo, jambo ambalo amesisitiza litawapa fursa wananchi wa nchi hiyo kujiamulia mustakbali wao.
Katika siku za hivi karibuni wananchi wa Afghanistan wamekuwa wakifanya maandamano makubwa katika miji tofauti ya nchi hiyo kupinga kitendo cha dharau cha askari wa Marekani dhidi ya matukufu ya Kiislamu, baada ya askari hao kuchoma moto Qur'ani Tukufu katika kambi yao huko Bagram. 961897
captcha