Nembo ya mji mtakatifu wa Madina kama, 'Mji Mkuu wa Kiutamaduni wa Ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2013' imezinduliwa na Abdul Aziz bin Majid, Amiri wa eneo la Madina.
Kwa mujibu wa gazeti la Al Watan la Saudi Arabia, nembo hiyo imezinduliwa baada ya kufanyika mashindano ya kuichora yaliyosimamiwa na kamati maalumu. Nembo iliyoshinda ina mnara wa Msikiti wa Mtume SAW na ramani ya ulimwengu wa Kiislamu.
Katika nembo hiyo kunaonekana nafasi ya mji wa Madina katika ulimwengu wa Kiislamu na pembizoni mwa ramani ya ulimwengu wa Kiislamu kuna hilali yenye maandishi yasemayo: 'Madina, Mji Mkuu wa Kiutamaduni wa Ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2013'.
Itakumbukuwa kuwa Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni (ISESCO) hivi karibuni liliidhinisha muswada wa kutangaza Madina kuwa mji mkuu wa ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2013.
Kila mwaka ISESCO hutangaza moja kati ya miji ya ulimwengu wa Kiislamu kuwa mji mkuu wa utamaduni kwa lengo la kushajiisha masuala ya utamaduni wa Kiislamu.
962090