IQNA

Wimbi la kupinga kuchomwa moto Qur'ani lawafukuza wafanyakazi wa UN Afghanistan

15:28 - February 28, 2012
Habari ID: 2282633
Wimbi kubwa la malalamiko ya wananchi wa Afghanistan dhidi ya kitendo kiovu cha askari wa Marekani cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu limewalazimisha wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo kuondoka Afghanistan.
Ripoti zinasema Umoja wa Mataifa kama zilivyofanya taasisi nyingine za kimataifa, umelazimika kuwaondoa wafanyakazi wake nchini humo kwa sababu za kiusalama kutokana na machafuko na mapigano yaliyosababishwa na kitendo kiovu cha askari wa Marekani katika kituo cha anga cha Bagram cha kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu.
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wameondoka katika mji wa Kunduz huku waandamanaji wakijaribu kuvamia ofisi za taasisi hiyo ya kimataifa.
Maandamano na malalamiko ya wananchi wa Afghanistan dhidi ya kitendo hicho kiuvu cha askari wa Marekani yangali yanaendelea licha ya kupita wiki moja sasa tangu askari hao wachome moto nakala za kitabu kitakatifu cha Qur'ani. 961962

captcha