IQNA

Semina ya 'Muujiza wa Qur'ani; Lugha ya Zama Hizi' kufanyika Jordan

15:18 - February 29, 2012
Habari ID: 2282670
Semina ya 'Muujiza wa Qur'ani; Lugha ya Zama Hizi' imepangwa kufanyika leo Jumatano huko Jordan. Semina hiyo imeandaliwa na Jumuiya ya Miujiza ya Qur'ani na Suna ya Jordan.
Kwa mujibu wa gazeti la ad-Dastur linalochapishwa Jordan, semina hiyo itafanyika kwa usimamizi wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Jordan katika Msikiti wa Shahidi Malik Muasis Abdallah wa Kwanza, ambao ni mashuhuri kwa jina la Msikiti wa Shahidi katika mji mkuu Amman.
Hutuba ya kikao cha ufunguzi cha semina hiyo ya Qur'ani kitakachoanza kesho saa kumi itatolewa na Abdallah al-Muslih, mhubiri mashuhuri wa Jordan. Atazungumzia suala la muujiza wa Qur'ani katika zama hizi.
Jumuiya ya Muujiza wa Qur'ani na Suna ya Jordan imewaomba Wajordan washiriki kwa wingi katika semina hiyo na imeandaa sehemu maalumu kwa ajili ya wanawake watakaohudhuria semina hiyo.
Jumuiya hiyo iliasisiwa nchini Jordan mwishoni mwa mwaka 2010 ambapo imekuwa ikijishughulisha na masuala mbalimbali ya utafiti kuhusiana na muujiza wa Qur'ani Tukufu.
Lengo la jumuiya hiyo ni kuwafahamisha wananchi wa Jordan kuhusiana na muujiza wa kitabu hicho kitakatifu pamoja na suna za Mtume ili kuwanufaisha watafiti na watu walio na hamu ya kujihusisha na mafundisho ya kitabu hicho cha mbinguni. 962320
captcha