IQNA

Chuo Kikuu cha Birmingham Kuandaa mashindano ya Qur'ani

15:20 - February 29, 2012
Habari ID: 2283074
Chuo Kikuu cha Birmingham cha Uingereza kinapanga kuandaa mashindano ya Qur'ani kwa wanachuo wa Kiislamu hapo tarehe 14 Machi.
Kwa mujibu wa tovuti ya ISOC mashindano hayo huandaliwa kila mwaka kwa ushirikiano wa Muungano wa Jumuiya za Wanachuo Waislamu FOSIS na kuwashirikisha wanachuo wa kike na kiume kutoka pembe zote za Uingereza.
Lengo la kufanyika mashindano hayo ni kuandaa uwanja wa kushirikiana zaidi wanachuo wa Kiislamu katika kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kuelewa zaidi mafundisho ya kitabu hicho kitakatifu.
Mashindano mengine kama hayo yaliandaliwa mwezi Juni mwaka uliopita katika Chuo Kikuu cha Cardiff katika jimbo la Wales nchini Uingereza ambapo washiriki walichuana katika makundi matatu ya kuhifadhi juzuu ya 30, sura ya Baqarah na hifdhi ya sura za Fatiha hadi An'am au sura za Yasin hadi an-Nas.
Katika kitengo cha kiraa pia washiriki walishindana kusoma sura mbili kati ya sura za ar-Rahman, Hashr, Mulk, Muzammil na Kiama na sura moja kati ya Yusuf, Ibrahim, Yasin, Qaf na Waqia. Muungano wa Jumuiya za Wanachuo wa Kiislamu FOSIS wa Uingereza uliasisiwa mwaka 1963 kwa lengo la kuhudumia maslahi ya wananachuo Waislamu wa vyuo vikuu vya nchi hiyo na Jamhuri ya Ireland. Muungano huo una matawi katika pembe tofauti za Uingereza. 962384
captcha