Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA kanda ya Afrika, makundi kadhaa ya wanawake Rwanda yanashiriki katika maonyesho hayo yatakayoendelea hadi Machi 8 na ambayo yanajumuisha harakati za kibiashara, kazi za mkono ushonaji nguo na ukulima. Maonyesho hayo ni kuhusu mafanikio ya Wanawake Waislamu katika kipindi cha miaka 17 iliyopita.
Akiwahutubia wanawake hao, Mufti wa Rwanda Sheikh Abdul Karim Gahutu amesema katika Qur'ani Tukufu wanawake wamepewa umuhimu mkubwa.
Ameongeza kuwa jamii ya Waislamu Rwanda ikishirikiana na serikali
inalenga kuinua nafasi ya wanawake nchini humo. Amesema kuna mpango wa kuwaelimisha wanawake Waislamu Rwanda kuhusu haki zao. Huku akiwapongeza wanawake kwa hatua walizopiga Mufti wa Rwanda amewataka kuimarisha juhudi zao na kulenga juu.
Aidha Mufti amewataka wanawake Waislamu Rwanda kutuma misaada kwa watu wa Somalia wanaokabiliwa na matatizo. Amesema ni jukumu la Kiislamu kuwasaidia wanaohitajia.
Mbunge mwanamke Muislamu Bi Saidat Mukanoheli pia amehudhuria maonyesho hayo.
962438