Akizungumza mjini Tehran Sayyid Mohammad Husseini ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali kitendo hicho cha wanajeshi wa Marekani cha kuichoma moto Qur'ani Tukufu. Huku akisema si mara ya kwanza Wamarekani kutenda kitendo hicho cha kishenzi, ameongeza kuwa vitendo hivyo vitapelekea Wamarekani wachukiwe zaidi kimataifa.
Dkt. Husseini ameongeza kuwa Qur'ani Tukufu ni moja ya vitabu vinavyouzwa kwa wingi zaidi duniani.
Wiki iliyopita wanajeshi vamizi wa Marekani walichoma moto kitabu kitakatifu cha Qur'ani katika kituo cha jeshi la anga cha Bagram nchini Afghanistan.
Maulamaa hao wa Kiislamu wamekemea vikali kitendo hicho kiovu cha askari wa Marekani na kusisitiza juu ya udharura wa jamii ya kimataifa kulinda matukufu ya dini mbalimbali.
962878