Kwa mujibu wa gazeti la Arab News, mashindano hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Saudia kwa usimamizi wa Salman bin Abdul Aziz, Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo yalianza tarehe 27 Februari. Mashindano hayo yameendelea kwa kushirikishwa washindani 51 wa kiume na 40 wa kike. Washindi wa mwisho watatangazwa baadaye leo na kutunukiwa zawadi nono. Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu kwa madhumuni ya kueneza na kutekelezwa mafundisho ya Qur'ani Tukufu katika maisha ya mwanadamu. 964494