Kwa mujibu wa gazeti la al-Yaum as-Sabe' kongamano hilo ambalo litafanyika chini ya anwani ya 'Nyimbo za Kidini' na kwa kauli mbiu ya 'Kupenda Misri' litawajumuisha viongozi wa kisiasa, kidini, kijamii na matabaka mbalimbali ya wananchi wakiwemo vijana. Miongoni mwa viongozi na shakhsia watakaoshiriki kwenye kongamano hilo ni pamoja na Mahmoud Uzb, mshauri wa Sheikh wa al-Azhar, Swifwat al-Bayadhi, mkuu wa Kundi la Injili la Misri, Samih Morris, kasisi mashuhuri wa Misri, Izzat Shakir na Askofu Mkuu wa Kanisa la Injili la Nasr. Askofu Izzat amesema kwamba uamuzi wa wanazuoni wa Kiislamu na Wakristo wa kukusanyika kwa ajili ya kuombea amani na utulivu wa Misri una umuhimu mkubwa. 964400