IQNA

Mfanyabiashara wa Misri aliyeuvunjia heshima Uislamu aachiwa huru

17:04 - March 04, 2012
Habari ID: 2285405
Mahakama moja ya Misri jana Jumamosi ilimwachilia huru Najib Sawaris mfanyabiashara Mkristo wa Misri aliyevunjia heshima Uislamu kwa madai kwamba mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake hayakuwa na msingi.
Hii ni mara ya pili kwa mfanyabiashara huyo tajiri kuondolewa mashtaka ya kufanya dharau dhidi ya matukufu ya kidini katika kipindi cha wiki moja. Siku ya Jumanne mfanyabiashara huyo alifutilia mbali mashtaka mengine kama hayo. Akifutilia mbali kesi iliyokuwa ikimkabili Sawaris, Jaji Janh Bulaq Abul Ala amesema kuwa mwendesha mashtaka mkuu wa Misri anafanya uchunguzi kuhusiana na tuhuma zilizotolewa dhidi ya mfanyabiashara huyo na kwamba hadi wakati matokeo ya uchunguzi huo yatakapotolewa hakuna mtu mwingine yoyote aliye na haki ya kuchunguza tuhuma hizo. Mfanyabiashara huyo hivi karibuni alichora vikatuni vya kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu kwenye ukurasa wake wa Facebook. 964520
captcha