Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Jordan ametuma mwaliko kwa nchi 40 za Kiarabu na Kiislamu kwa ajili ya kushiriki kwenye mashindano ya 20 ya kimataifa ya hifdhi, kiraa na tafsiri ya Qur'ani Tukufu.
Akibainisha suala hilo, Abdul Salaam al-Ibadi, Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Jordan amesema kuwa mashindano hayo yatafanyika katika makundi matatu ya hifdhi ya Qur'ani nzima na tafsiri, hifdhi ya juzuu 20 na hifdhi ya juzuu 10. AL-Ibadi ameongeza kuwa washindani wa kike watakaoshiriki mashindano hayo yatakayofanyika katikati mwa mwezi wa Rajab watasimamiwa na Rania Abdallah, mke wa mfalme wa Jordan. Hatua ya mwisho ya mashindano hayo imepangwa kufanyika katika kumi la mwisho la mwezi mtukufu wa Ramadhani. Washindi watatunukiwa zawadi na mfalme wa Jordan katika sherehe maalumu itakayofanyika usiku wa Leilatul Qadr. 964761