Kituo cha uchapishaji Qur'ani na vitabu ningine vinavyohusiana na kitabu hicho kitakatifu kitajengwa hivi karibuni huko Ajman, ufalme mdogo zaidi kati ya falme saba zinazobuni Umoja wa Falame za Kiarabu au kwa jina jingine Imarati.
Kwa mujibu wa tovuti ya Gulf News, Sheikh Hamid bin Rashid an-Naimi, mfalme wa ufalme huo tayari ametoa amri ya kujengwa kituo hicho. Mbali na kuchapisha Qur'ani Tukufu na vitabu vilivyo na uhusiano na kitabu hicho kitakatifu, kituo hicho pia kitakuwa kikichapisha tarjumi za Qur'ani kwa lugha tofauti. Kuanzisha uhusiano na taasisi nyingine za Qur'ani na kueneza ujumbe wa Qur'ani Tukufu pamoja na kutekelezwa ratiba tofauti zinazohuisana na kitabu hicho cha mbinguni ni malengo mengine ya kuanzishwa kituo hicho. 964960