Kwa mujibu wa tovuti ya albirr.com, mashindano hayo yanaandaliwa na Taasisi ya Albirr ya Uingereza.
Mashindano hayo yatakuwa na vitengo vitatu vya kuhifadhi Qur'ani kamili kwa wale wenye umri wa miaka 22 au chini, kuhifadhi Juzuu 20 kwa walio na umri wa miaka 18 na chini na kuhifadhi juzuu 10 kwa walio na umri wa miaka 14 na chini.
Mashindano hayo ni wazi kwa wale tu wanaoishi daima Uingereza.
Zawadi za kifedha za hadi Pauni 5000 zitatolewa kwa washindi wa vitengo mbali mbali.
Taasisi ya Albirr ya Uingereza hujishughulisha na utoaji misaada na shughuli za Qur'ani kwa lengo la kuwawezesha wanaotaka kujifunza kitabu hiki kitakatifu kufanya hivyo kwa njia sahali.
Taasisi hii husambaza nakala za Qur'ani na vitabu vingine vya Kiislamu bila kupokea malipo. Taasisi ya Albirr pia inalenga kuimarisha utamaduni wa kusoma, kufahamu na kuhifadhi Qur'ani Tukufu miongoni mwa watoto Uingereza.
965691