IQNA

Wasichana waliohifadhi Qur'ani waenziwa Uturuki

13:41 - March 05, 2012
Habari ID: 2285920
Nchini Uturuki, wasichana waliohifadhi Qur'ani wameenziwa katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Oovtadh mjini Nuchehar.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, hafla hiyo ilianza kwa kisomo cha Qur'ani Tukufu na kuendelea kwa hotuba ya Mufti wa mji huo Sheikh Ya'qub Azturk ambaye alibainisha fadhila za kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Ameashiria aya za Qur'ani na Hadithi za Mtume SAW kuhusu umuhimu wa kusoma na kuhifadhi Qur'ani.
Amewapongeza walio hifadhi Qur'ani, wanafunzi na wafanya kazi wa kituo hicho.
Wasichana saba bora waliohifadhi Qur'ani wametunukiwa zawadi.
Darsa maalumu za kutoa mafundisho ya kuhifadhi Qur'ani kikamilifu hutolewa zinahudhuriwa na wasichana 170 katika kituo hicho.
964501
captcha