IQNA

Iran yaanzisha harakati ya utafiti wa Qur'ani katika tiba na afya

13:41 - March 05, 2012
Habari ID: 2285940
Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema wizara hiyo imeanzisha harakati ya utafiti wa Qur'ani katika setka za tiba na afya.
Daktari Bi Mardhiya Wahid Dastjerdi amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa wizara yake inalipa umuhimu mkubwa suala ya utafiti wa Qur'ani katika sekta ya matibabu kwa lengo la kutoa muelekeo kuhusu tiba kwa mtazamo wa Qur'ani na Hadithi.
Amesema taasisi za utafiti wa Qur'ani zimeanzishwa katika vyo vikuu vya sayansi za tiba kote Iran na kuongeza kuwa, vyuo vikuu vyote vya sayansi za tiba vinatakiwa kuandaa kwa uchache kongamano au semina moja kila mwaka kuhusu utafiti wa Qur'ani na tiba.
Daktari Bi.Wahid Dastjerdi amesema tayari wizara yake imeshaandaa Mkutano wa Kwanza wa Utafiti wa Qur'ani na Tiba ambao ulifanyika katika mji mtakatifu wa Qom ambapo Ayatullah Nasser Makarem Shirazi alihudhuria. Amesema mkutano mwingine sawa na huo utafanyika katika kipindi cha miezi michache ijayo.
965246
captcha