Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharq la Qatar mashindano hayo yaliyoratibiwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Turathi ya Qatar yalihudhuriwa na zaidi ya taasisi na vituo vya Qur'ani 14. Yalianza tarehe 26 Februari. Akifafanua suala hilo Jamal Faiz mkuu wa kitengo cha utamaduni cha Idara ya Shughuli za Vijana inayofungamana na Wizara ya Utamaduni ya Qatar na ambaye alisimamia kamati za mashindano hayo amesema kuwa idara yake imewaandalia washindi wa mashindano hayo zawadi nono ambazo watapewa katika sherehe maalumu. Amesema zawadi hizo zitatolewa kwa lengo la kuwashajiisha vijana zaidi wazingatie Qur'ani na kujipamba kwa thamani za kitabu hicho cha mbinguni. Mkuu huyo wa Kamati ya Mashindano ya Qur'ani na Hadithi ya Qatar amesema washindi wa mashindano hayo wataiwakilisha Qatar katika mashindano ya kieneo ya nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi ambayo yamepangwa kufanyika mwezi Oktoba huko katika mji mtakatifu wa Madina. 965536