Kwa mujibu wa shirika la habari la Imarati WAM, kituo hicho kitakachokuwa huru kuendesha shughuli zake kitahusika na masuala ya mafunzo ya hifdhi ya Qur'ani na masomo mengine yanayohusiana na kitabu hicho. Adil Jumua' Matar Mkuu wa Ofisi ya Taasisi za Kiislamu na Idara ya Masuala ya Kiislamu na Kheri ya Dubai amesema kuhusiana na suala hilo kwamba kituo hicho kitaanza shughuli zake baada ya kusajiliwa rasmi. 965646