IQNA

Waislamu watakiwa kufuata mafundisho ya Qur'ani

10:09 - March 07, 2012
Habari ID: 2287156
Kaimu Waziri wa Awqaf na Masuala ya Kidini Pakistan Haji Ehsanuddin Qureishi amesema suluhisho la matatizo yote yanayowakumba Waislamu liko katika kufuata mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Qureishi ameongeza kuwa, 'Tunaweza kutatua matatizo yetu ya kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa kutekeleza maamurisho ya Allah SWT'.
Ameyasema hayo katika ufunguzi wa maonyesho ya Qur'ani Tukufu katika Kituo cha Utamaduni cha Iran mjini Islamabad siku ya Jumatatu Machi sita.
Hafla hiyo imehudhuriwa na mkurugenzi wa kituo hicho Abbas Famuri, Mhariri Mkuu wa Gazeti la Daily Pakistan Mujeeb-ur-Rahman Shemi kati ya wengine.
Qureishi amesema maonyesho ya Qur'ani Tukufu ni hatua inayostahiki kupongezwa kwani inawapa fursa Waislamu kutizama nakala mbali mbali za Qur'ani Tukufu.
966694
captcha