IQNA

Kongamano la Qur'ani na Ahul Bayt AS

10:47 - March 07, 2012
Habari ID: 2287210
Chama cha Majlis Wahdat Muslimeen ya Pakistan kimetangaza kuwa itaandaa kongamano la 'Qur'ani na Ahul Bayt AS' baadaye mwezi huu wa Machi.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Maulana Raja Nasir Abbas Jafri amesema lengo la kongamano hilo ni kuwaunganisha Waislamu wa Pakistan ili waweze kukabiliana na uingiliaji wa Marekani nchini humo.
Akiwahutubia waandishi wa habari siku ya Jumatatu, Maulana Jafri ametoa wito kwa wafuasi wa madhehebu yote ya Kiislamu kuhudhuria kongamano hilo litakalofanyika katika ukumbi wa Nishtar Park mjini Karachi mnamo Machi 25.
Maulana Jafri amesema vibaraka wa Marekani ndio ambao wamekuwa wakiwaua Mashia mjini Karachi. "Wako miongoni mwetu na wanawahudumia Wamarekani,"amesema akiwaashiria magaidi wanaowaua Mashia.
Amesema hakuna chuki baina ya Masuni na Mashia na kwamba vibaraka wa Marekani ndio wanaoibua hitilafu.
966701
captcha